HATUA ZA KUHARAKISHA MAFANIKIO YAKO.

1. Bobea Kwenye Jambo Fulani (Specialisation). 

Amua kuwa na ujuzi na uwezo wa kipekee katika eneo fulani la maisha yako.

Kila aliyefanikiwa hata kama anafanya mambo 10 lazima kuna jambo moja ambalo watu wanamfahamu zaidi kwa hilo.

Hii ndio maana ukifikiria au likitajwa jina la mtu yoyote aliyefanikiwa lazima utaweza kutaja kitu kimoja kinachomtambulisha.

Kama wewe bado haujapata kitu cha kukutambulisha kimoja ambacho jina lako likitajwa kila mtu anaweza kukisema basi inabidi ufanye hivyo.

Hebu fikiria nikitaja majina haya:

Mike Tyson, Serena Williams, Justine Bieber, Bill Gates, Mbwana Samatta.

Je, unawaza kitu gani kuhusu wao?.

Mafanikio Huanza pale unapoamua kuwa na kitu kimoja kikubwa kuliko vyote.

2. Fanye Kitu cha Tofauti (Differentiation).

Amua kufanya Kitu ambacho aidha hakifanyiki au ukifanye kwa njia tofauti.

Lazima kuwe na utofauti kati ya unachofanya (What) au unavyofanya (How) na wengine.

Kama unafanya kile wanachofanya wengine ama kama wanavyofanya basi hauna haki ya kufanikiwa.

Jiulize - Kuna tofauti yoyote na wengine kwa HIKI ama HIVI ninavyofanya?

3. Amue Unataka Kuwafikia Watu wa Namna Gani (segmentation).

Amua unachofanya, unachouza unalenga kundi gani la watu.

Huwezi kumfanya kila mtu kuwa mteja wako.

Amua unataka kuwafikia watu wa namna gani na jikite katika soko lako.

4. Uwekeze Nguvu Zote na Muda Wote Kwenye Jambo Hilo (Concentration).

Usitapanye muda au nguvu zako kwa mambo mengine, jikite kufanya ulichoamua.

Usiwe mtu unayetamani kufanya kila kitu.

Kuna wengi wanafeli kwa sababu wamekosa mwelekeo, kila kitu wamo.

Hebu amua kuanzia leo unawekeza rasilimali zako katika jambo gani la maisha yako.

Acha kutapatapa, utachelewa kufanikiwa.



Comments

Popular posts from this blog

USHINDE UTUMWA KIZUIZI CHA MAFANIKIO YAKO

Zero To One by Peter Thiel Book Summary & Review